Sunday 28 April 2013

MSHUKIWA WA MABOMU YA BOSTON AHAMISHIWA JELA!!!


Maafisa wa Marekani wanasema mshukiwa wa mabomu yaliyolipuliwa wakati
wa Boston Marathon,  Dzhokar Tsarnaev amehamishiwa kwenye kituo cha afya katika jela ya  serikali kuu kutoka hospitali ambapo alikuwa akipata matibabu kwa majeraha aliyopata wakati alipokamatwa wiki iliyopita.

Idara ya usalama ya Marekani ilisema Ijumaa kwamba Tsarnaev  alihamishiwa kwenye kituo cha afya cha  serikali kuu  cha Devens kwenye eneo la  kituo cha jeshi huko Fort  Devens, katika jimbo la Massachusets.

Msemaji hakutoa taarifa juu ya hali ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 19, ambapo maafisa wamesema anapata matibabu ya jeraha lake la shingo. Idara ya magereza imesema eneo la Devens ni jela ambayo   inatoa  matibabu ya hali ya juu au ya muda mrefu kwa wafungwa.

Kaka wa mshukiwa na mshiriki  katika ulipuaji mabomu,Tamela Tsarnaev alifariki katika mapigano na Polisi usiku wa alhamisi wiki iliyopita.

Maafisa wa New York wanasema washukiwa hao walikuwa wakipanga mashambulizi huko Times Square wakati wakikimbia maafisa. Mkuu wa Polisi wa New York Ray Kelly  anasema Dzokhar aliwaambia wachunguzi walipanga waende  New York ili kulipua milipuko yao iliyobaki.

No comments:

Post a Comment