Friday 19 April 2013

MSHUKIWA WA KWANZA AUAWA ,WA PILI HAJULIKANI ALIKO !!!

Polisi na maafisa wa ujajusi wa FBI nchini Marekani wanaendeleza msako mkubwa dhidi ya mshukiwa wa pili wa mashambulizi ya Boston baada ya mshukiwa wa kwanza kuuawa Ijumaa asubuhi kwa kupigwa risasi.

Naye mshukiwa wa pili ambaye anafahamika kwa jina la Dzhokhar Tsarnaev mwenye umri wa miaka 19 alifaulu kukwepa ufwatuliaji huo wa risasi na hakulikaji aliko kwa sasa.



Aidha, vyombo vya usalama vinasema kuwa mmoja wa washukiwa aliyeuawa alikuwa kakake mshukiwa wa pili na alikuwa na umri wa miaka miaka 26 na wote ni raia wa Chechen.

Imebainika kuwa mshukiwa huyo alipoteza maisha akiwa kizuizini baada ya kupigwa risasi na badaye kuzuiliwa mjini Boston.

Awali, maafisa wa Ujasusi wa FBI walitoa picha za washukiwa wawili wanaotuhumiwa kutekeleza mashambulizi hayo wawili. Shughuli za usafiri katika mji wa Boston na maeneo hirani zimesimama huku watu wakisalia ndani ya nyumba zao.

Picha za washukiwa hao zilitolewa kupitia kanda za usalama za CCTV zikionesha wanaume wawili wakiwa wamevaa nguo nyeusi, kofia za mchezo wa baseball na wakiwa na mifuko migongoni.


Richard DesLauriers mmoja wa maafisa wa FBI amesema kuwa washukiwa hao ni hatari sana na wananchi wa Marekani hawastahili kuwakaribia.

Mepema juma hili, FBI ilitoa picha za kifaa cha jikoni kilichotumiwa kutekeleza mashambulizi hayo pamoja na washukiwa hao wakitupa mifuko yao katika eneo la kumalizia mbio hizo ndefu.

Mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya watu watatu na kuwajeruhi wengine 170 wakiwemo watoto watatu ambao madaktari wanasema hali yao bado haijatengemaa.

Rais Barrack Obama amesema kuwa waliohusika na mashambulizi hayo watachukuliwa hatua kali za kisheria huku akiwahakikishia familia za walioathirika kuwa serikali iko pamoja nao wakati huu mgumu.

Siku ya Alhamisi rais Obama alizuru Boston na kuhudhuria ibada ya wafu ya watu watatu waliopoteza maisha yao na kuwaombea pia wale wanaopata matibabu Hospitalini.

Ibada hiyo pia ilihudhuria na Mitt Romney aliyekuwa mgombea urais nchini humo wakati wa uchaguzi Mkuu mwaka uliopita.

No comments:

Post a Comment