Friday 19 April 2013

CHAMA CHA WANASHERIA ZANZIBAR ZLS

Chama Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) kinapenda kukujulisheni na kukuarifuni kwamba kimeandaa Kongamano la Wazi (Public Lecture) lenye lengo la Kuzungumzia "Mchakato wa Katiba Mpya na Mustakabali wa Muungano katika kuadhimisha Sherehe za kutimiza miaka 49 ya Muuungano kati ya Tanganyika na Zanzibar"

Kongamano linatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 20/04/2013 hapo kesho kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa 7: 00 mchana katika ukumbi wa Taasisi uliopo katika Kampasi ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Vuga -Zanzibar.

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Othman Masoud Othaman (Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar) na mtoa mada ni Bwana Ali Uki (Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar).

Hivyo basi, nichukue fursa hii kukualikeni Rasmi na Kuwaomba muhudhurie kwa wingi bila ya kukosa ili tuweze kufikia lengo.

Tunatanguliza Shukurani zetu za dhati kwa Mashirikiano yenu tunakuombeni mje kusikiliza wataalamu wetu wanasheria watakavyotueleza namna ya mambo ya Muungano na Mustakabali wake. Karibuni sana wanawake kwa wanaume bila ya kuwakosa vijana wazee msikose kuhudhuria. 

No comments:

Post a Comment