Monday 15 April 2013

INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAJIUNN ,MSANII MKONGWE WA TARABU ZANZIBAR Haji Mohammed Amefariki Dunia



Habari tulioipata sasa hivi Kuwa Msanii Mkongwe na Muziki wa Taraab wa Kikundi cha Taraab cha Menlody East Africa Haji Mohammed Kijikuu cha Siti Bint Saad, amefariki dunia wakati akipelekwa katika hospitali ya Muhimbnili baada ya kuzidiwa na Presha asubuhi ya leo. 

Majira ya saa nne Marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya sukari kwa muda mrefu na presha, mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa mchana huu na boti ya Kampuni ya Azam Marine saa 3.45 jionoo kwa ajili ya maziko yatafanyika Mjini Zanzibar.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Menlody Hashim Salum amesema amezungumza na marehemu asubuhi na kwambwambia anakwenda hospitali kuonanana Daktari wake,, na kushtuka kupatahabari ya Msiba huo majira ya saa 4,asubuhi.

Marehemu Haji Mohammed ameacha mke na watoto, watatu
Mungu amlaze Pema Peponi Amani.





No comments:

Post a Comment