Tuesday 9 April 2013

AL SHABAAB WATOWA MADAI MAZITO !!!

"Nyaraka hizo zina habari za siri za hali ya juu, ikiwa ni pamoja na
 ripoti za kiintelijensia, mawasiliano ya ndani, maelezo kwa urefu kuhusu
operesheni zilizopangwa na mambo mengine ya siri," ofisi ya habari ya
al-Shabaab ilisema katika taarifa iliyotolewa tarehe 3 Aprili kupitia Twitter.

Kikundi kilidai kuwa baadhi ya nyaraka zilizotoa ni pamoja na barua kutoka
 kwa "utawala wa Kiarabu wenye ushawishi" kwa raisi wa Somalia
unaomwambia kuwa "ateue watu fulani kwa nafsi maalum ndani ya serikali
 yake ili kurahisisha mashirikiano mazuri na kubadilishana habari za

 kiintelijensia baina ya nchi hizo mbili".

"Tutachapisha baadhi ya nyaraka katika Twitter ndani ya saa zijazo na
 nyingine tutazichapisha itakapoonekana inafaa, Mungu Akipenda,"
 taarifa hiyo ilisema.

Takriban wiki moja baadaye, bado al-Shabaab hawajatuma kwenye Twitter
nyaraka kama hizo.

Hata hivyo, waraka wenye tarehe 27 Machi unaodaiwa ni kutoka serikali ya
 Qatar unaopendekeza kwamba afisa wa Somalia ateuliwe kuwa
 mkuu wa operesehni za kiintelijensia, ulitumwa katika ukurasa wa habari
 wa tovuti ya Somalia tarehe 30 Machi. Uhalisia wa waraka huo haukuweza kujulikana, na
 wala kuthibitishwa kwamba ilikuwa moja ya nyaraka ambazo
 al-Shabaab wanadai kuwa nazo.

"Al-Shabaab wanajulikana kwa mchezo mchafu na sasa wanachagua kila
 mbinu chafu inayopatikana ili kupotosha maoni ya umma wa Somalia,"
 alisema Abdiwahab Mohamed, mchambuzi wa masuala ya kisiasa
aliyeko Mogadishu, na ambaye pia ni mhadhiri wa chuo kikuu.

Kikundi hakiwezi kuingia katika siri za serikali, na lengo nyuma ya kufanya
 madai hayo ya uongo ni kunyanyua ari ya wapiganaji waliotupwa wa
al-Shabaab, aliiambia Sabahi.

"Al-Shabaab siku zote wamekuwa wakisema uongo kupitia uenezaji wa madai
yasiyo na msingi," alisema. "Madai yao ya mwisho kwamba yamepata nyaraka za
 siri kutoka kwa ofisi ya raisi, kwa kweli, ni sehemu ya propaganda ambayo
 kikundi hiki kimeunda dhidi ya serikali ya Somalia."

Al-Shabaab 'waachana na ukweli'
Madai ya uongo ya al-Shabaab ya kuwa yamepata nyaraka za siri ni
uthibitisho kwamba kikundi kimekuwa dhaifu katika kukusanya
habari za kiintelijensia na sasa kumeamua kueneza uongo na hatua
 nyingine za kukata kwa tamaa ili kuficha nyuso zao, alisema
 Faisal Osman, mchambuzi wa kisiasa za Somalia anayesimamia
 kikundi cha wanamgambo.

"Madai ya al-Shabaab ya kuweza kuifikia ofisi ya raisi ni ya uongo na
 yanaonyesha majaribio ya kikundi ya kukata tamaa ili kupindisha nadhari
za watu kutoka kushindwa kwao mfululizo katika uwanja wa vita,"
 Osman aliiambia Sabahi.

"Baada ya kuwa al-Shabaab wamedhoofishwa kijeshi na kushindwa katika
 uwanja wa mapambano, kinatafuta kujionyesha kama kikundi
 kilichoungana
 na chenye nidhamu ambacho kina uwezo wa kiintelijensia ambao
 usingepaswa kudharauliwa," alisema. "Kwa kweli, hata hivyo, kiko
dhaifu kimsimamo wa operesheni na njia zao za kukusanya habari za
 kiintelijensia."

Abdirahman Mohamud, mchambuzi wa siasa anayefuatilia vikundi
vyenye siasa kali, alisema kuwa madai ya uongo ya al-Shabaab ni
"pigo kubwa kwa kuaminika wa kikundi".

"Wale wenye dhamana ya chombo cha propaganda cha kikundi ni
wapuuzi sana kwa vile wasingeweza hata kugundua waraka huu, ambao
wanauita wa siri na ambao ulipenya kutoka afisi ya raisi, ni huu ambao
ulitumwa siku kadhaa kabla katika tovuti nyingine za Somalia," alisema.

 "Hii inaonyesha kwamba watu hawa wametengana kabisa na ukweli."

Ahmed Aden mwenye umri wa miaka 58 na mtumishi huko Hiran, alisema
 kuwa kwa muda mrefu al-Shabaab wamekuwa na tabia ya kusema uongo
 katika vyombo vyao vya habari vya kampeni, kwa hivyo hakuna yeyote
 anayeamini madai yaliyotolewa na kikundi hicho cha wanamgambo.

"Tabia za al-Shabaab ziko mbali na mantiki yoyote kwa kuwa kikundi hiki
kimezoea kusema uongo katika njia mbaya sana," Aden aliiambia Sabahi.
 "Aina hii ya propaganda mbaya zitakwama na hakuna mtu atakayesikiliza
 kikundi hiki."

Kikundi cha wanamgambo kimeshindwa kuzipata nyoyo na akili za
watu wa Somalia kwa sababu kimekuwa kikiwashambulia raia wasio na
 hati ya mfululizo kwa milipuko ya mabomu na mauaji ya kulenga, alisema.



No comments:

Post a Comment