Tuesday 9 July 2013

KARIBU MWENZI MTUKUFU WA RAMADHAN !!!

Hakukuthibitishwa kuonekana mwezi kisheria, na kwa hivyo leo jumanne 9 julai 2013 tunakamalisha Shaaban. Ramadhani itaanza kesho InshaAllah Jumatano 10 julai ambayo itakuwa Ramadhan mosi 1434 InshAllah.
Tunamuomba Allah Tala atuwafikishe kupata maghfira na baraka za Ramadhan sote umma mzima - Ameen

Friday 5 July 2013

USALITI WA CCM ZANZIBAR ZIDI YA WAZANZIBAR WENZIWAO !!!


Tarehe 2/07/2013 Chama Cha Mapinduzi –CCM walifanya kikao katika ofisi yao Kisiwanduwi ambacho kiliongozwa na Naibu Katibu Mkuu CCM Vuai Ali Vuai.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria katika kikao hicho ni :

• Yussuf Masauni( Mkurugenzi wa mambo ya nje wa CCM na mbunge wa Jimbo la Kikwajuni.)

• Sadifa Juma Khamis ( Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana –CCM, Mbunge wa jimbo la Donge, na mjumbe wa kamati kuu ya CCM.)

• Mwakilishi mmoja (1) kutoka Makao makuu ya CCM.

• Mihayo (Mwenyekiti wa Mkoa wa Vyuo vya Zanzibar).

WALIOITWA NA WALENGWA WA KIKAO HICHI NI:-

Viongozi wa ZAHLIFE (Umoja wa Vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu Zanzibar). Viongozi wa umoja huo ambao walihudhuria katika kikao hicho ni :-

1) BAKARI KHATIBU (Chuo cha Afya -Mbweni)
2) ABDUL-KAREEM (Chuo cha Afya -Mbweni)
3) SIMAI HAJI (Chuo cha Uwalimu –Chukwani)
4) KINANA ( Chuo cha Utalii)
5) ZEYANA (SUZA)
6) RAJAB (Zanzibar University -TUNGUU)

(TUNAOMBA MAJINA KAMILI KWA WANAOWAFAHAMU VIZURI VIJANA HAWA ili tuyaandike kwa ukamilifu).

AGENDA ZILIZOZUNGUMZWA:

Mwenyekiti wa kikao hicho Vuai Ali Vuai aliwasilisha mada kwa vijana hao akidai kuwa ni maagizo kutoka kwa Rais wa Zanzibar Mhe, Ali mohammed Shein.

i. Kwanza aliwataka viongozi hao wa ZAHLIFE waisaidiye CCM katika kwenda kinyume na kuyapinga matakwa ya wazanibari ya kudai mamlaka kamili kupitia mabaraza ya katiba ya taasisi hiyo.
Aliwahakikishia kuwa gharama zote za vikao, posho, na kila kitu kitalipwa na Mhe. Shein chini usimamizi wake Vuai Ali Vuai.

ii. Pili aliwataka wawaandae vijana wao wa vyuo vikuu katika kongamano maalumu litakaloitwa na CCM kesho Jumamosi ambalo litafanyika katika Ukumbi wa Bwawani ili waje wapewe nafasi ya kuchangia kwa kutoa maoni ya kupinga madai ya MAMLAKA KAMILI kwa Zanzibar.

iii. Aidha, viongozi hao wa vyuo vikuu vya Zanzibar walitakiwa kuandaa hotuba fupi ya kupinga madai ya mamlaka kamili kwa Zanzibar ambayo watatakiwa kuitoa jukwaani katika mkutano wa hadhara wa CCM utakaofanyika Jumapili hii katika viwanja vya kibanda maiti.
Hiyo ndio hali ilipofikia, Jiba limewasakama wasioitakia mema nchi yetu, waliokosa uzalendo kwa tama zao binafsi, wasioona haya wala vibaya kutaka kumaliza kuiuza Zanzibar yetu tuipendayo.

HATUA ZA KUCHUA KWA WAZANZIBARI

a) Taafifa hii isambazwe katika mitandao yote ya kijamii,

b) Wazanzibari wote wahudhurie kwa wingi katika KONGAMANO litakalofanyika kesho Jumamosi, tarehe 06/07/2013 asubuhi ili kupinga na kupaza sauti kwa pamoja kukataa unafiki utakaowasilishwa na vijana hao wa ZAHLIFE.

c) Viongozi wote wa CCM na wanavyuo wasaliti watangazwe ili kila mtu awajuwe.

ZANZIBAR KWANZA.