Sunday 31 March 2013

FAIDA YA VITUNGU MAJI !


Baadhi ya magonjwa ambayo hadi sasa haijafahamika tiba yake katika hospitali zetu yanayotibika kwa kitunguu maji ni pamoja na saratani (Cancer), kisukari, vidonda vya tumbo, presha, na pumu. Dawa hii pia ni tiba ya kifua kikuu.
Assalaam Alaykum mpenzi msomaji;  leo nitazungumzia tiba ya magonjwa mbalimbali kwa kutumia kitunguu maji.
Mbali ya kitunguu maji kutumika kama kiungo katika mboga zetu, lakini pia ni tiba inayotumika sana nchini Misri na imeonesha mafanikio kwa kutibu maradhi mbalimbali, yakiwemo yale yasiyo na tiba katika hospitali nyingi hapa nchini.
Baadhi ya magonjwa ambayo hadi sasa haijafahamika tiba yake katika hospitali zetu yanayotibika kwa kitunguu maji ni pamoja na saratani (Cancer), kisukari, vidonda vya tumbo, presha, na pumu. Dawa hii pia ni tiba ya kifua kikuu.
Kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali wa masuala ya tiba, kitunguu maji kina uwezo wa kufungua hamu ya kula, hutia kiu, hulainisha chakula tumboni na huleta hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume na wanawake.
Aidha mtaalamu mmoja anayefahamika kwa jina la Ibn Baitar amepata kunukuliwa akisema kwamba, kitunguu maji huingiza kwa wingi vitamin C katika mwili wa binadamu ambayo inasaidia sana kuona vizuri.
Lakini pia ndani ya kitunguu maji zimo chembechembe zenye kuua vijidudu (Bacterias) na ndio maana dawa hii ina uwezo pia wa kutibu kifua kikuu (TB), kaswendwe na kisonono.
Hivyo kupitia makala yetu haya, tunawashauri watu wapendelee sana kutumia kitunguu maji kwa ajili ya kinga na tiba ya maradhi katika miili yetu.
Na imethibitika kuwa wagonjwa wengi waliowahi kutumia tiba ya kitunguu maji kwa muda mrefu wamepata nafuu na wengine hupona kabisa maradhi yao.
Sasa ebu tuangalie matumizi sahihi ya dawa ya kitunguu maji;
Kwa mgonjwa wa kifaduro, pumu, vidonda vya tumbo, presha, kifua kikuu, malaria na ugonjwa wa matumbo (typhold) anatakiwa mgonjwa kuchukua juisi ya kitunguu maji ujazo wa kikombe cha kahawa achanganye na asali mbichi ujazo wa nusu lita, kisha aitumie kwa kula katika ujazo wa kijiko kikubwa asubuhi na jioni.
Ama wale wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo ya nguvu za kiume wanashauriwa watafune kitunguu maji kibichi kwa muda wa siku saba asubuhi na jioni.
Na maradhi yote yaliyobakia yanatibika kwa njia mbili zifuatazo;- kwanza kwa njia ya kiungo katika mboga na pili ni kwa kutafuna kitunguu chenyewe kila siku na Mola Muumba akipenda matatizo yatapungua ama kwisha kabisa.
Aidha kwa mgonjwa wa mapunye na kunyonyoka nywele kichwani anaweza kujitibu kwa kukipondaponda vizuri, alafu achanganye na mafuta ya zaituni, kisha apake kichwani mpaka atakapoona tatizo limekwisha.

mshikiwa wa kesi ya bapri Mushi Zanzibar



  Kisa nini hata kupewa hiyo kesi mimi sijuwi ,zaidi lakini ingiya kwenye YOU TUBE,Kongamano tarehe 01/14/2012 bwawani zanzibar 3

KWA HALI HII JAPANI SIENDI


ANAYEDAIWA KUMUUA PADRI MUSHI KIZIMBANI KESHOKUTWA




ALIYEKUWA mgombea wa uwakilishi jimbo la Rahaleo, Unguja kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Omar Mussa Makame (37) atafikishwa mahakamani Aprili 2, mwaka huu kwa tuhuma za kumuua Padri Everistius Mushi wa Kanisa la Romani Katoliki, Zanzibar.

Mwanasiasa huyo alikamatwa na maafisa wa upelelezi, kufuatia taarifa za siri na baadae kutambuliwa mara mbili katika gwaride maalum ambalo liliwahusisha watu walioshuhudia mauaji hayo Februari 17, mwaka huu Kisiwani humo.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Hamad Masoud Hamad alithibitisha kuwa Makame ni mwanachama wa chama hicho na alikuwa mgombea wao katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Rahaleo yanaonyesha kuwa Omar (CUF) alipata kura 2310 ambapo mgombea wa CCM Nassor Salum Ali alipata kura 3952:

“Taarifa za kukamatwa Omar ni mpya kwa upande wetu kama Chama cha siasa, tukio lenyewe kiuhalisia halina uhusiano na Chama chetu,”alisema Masoud ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, kabla ya kujiuzulu mwaka jana.

Hata hivyo, Masoud alisema kwamba kama Chama cha siasa, kitakaa na kumjadili kwa kina hatimae kitatoa msimamo wake kuhusiana na tukio hilo.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema jalada la uchunguzi wa kesi hiyo tayari limekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP) na siku ya Jumanne ijayo, atafikishwa mahakamani.

Alisema mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Mwanakwerekwe shehia ya Mwanakwerekwe mbali na shughuili za siasa ni fundi seremala.

Alisema mchoro wa mtu huyo anayedaiwa kuhusika na tukio hilo uliwasilishwa Polisi kabla ya kukamatwa kwake, hatimae kutambuliwa katika gwaride maalumu.

Wakati huohuo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kwa upande wake kimesema kukamatwa kwa watu wanaoshukiwa kuwahujumu viongozi wa Dini kutaondoa hali ya wasiwasi kwa wananchi na waumini wa madhehebu ya Dini mbalimbali, Zanzibar.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC (CCM) Zanzibar, Itikadi na Uenezi, Waride Bakari Jabu alisema wananchi walianza kupoteza imani na vyombo vya usalama wa raia kutokana na mfululuzo wa matukio bila ya wahusika kukamatwa.

CHANZO beltelraas.blogspot.nl

Friday 29 March 2013

North Korea declares it's 'combat ready'


                           Muda wowote kuanziya sasa kinaweza kuwaka huko !

SEVERAL DIE AS BUILDING COLLAPSES IN DAR ES SALAAM MARCH 29, 2013


 
              TUKO NYUMA SANA KIUOKOZI TUKITAKA TUSITAKE ! TUTAFUKIWA SANA NA KIFUSI KWA HALI HII

BREAKING NEWS

Taarifa zilizotufikia ni kwamba jengo lenye ghorofa 16 lililokuwa bado linaendelea kujengwa katika makutano ya barabara ya Indira Gandhi na Morogoro jirani na Burhani limeanguka. Inasemekana katika jengo hilo kulikuwa na watu takribani 60 ambao wanahofia kupoteza maisha. Taarifa kamili zitawajia hivi punde.

JAJI ATOWA TAMKO ZITO KESI YA UAMSHO

 Mzee Ibrahim, kuwasilisha kwa maandishi sababu za kufunga dhamana ya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki) ndani ya wiki mbili kuanzia jana.

Agizo la mahakama hiyo lilitolewa jana na Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Fatma Hamid Mahmoud.
Jaji Fatma alitoa uamuzi huo baada ya kukamilisha kusikiliza pande mbili kuhusu hatua ya dhamana ya washtakiwa hao 10 kufungwa na DPP kwa kutumia sheria ya Usalama wa Taifa ibara ya 19 (3) d sura ya 47 ya mwaka 2002.

Jaji Fatma alisema kwamba baada ya kupitia kumbukumbu za mwenendo wa kesi ya msingi, anaona upande mmoja dhamana imefungwa, lakini bado upande wa pili anaona dhamana iko wazi dhidi ya washtakiwa hao.

“Upande wa DPP muwasilishe kwa maandishi sababu zenu kwa nini washtakiwa wasipewe dhamana ndani ya wiki mbili,” alisema Jaji Fatma.

Aidha, alisema kwamba dhamana ni haki ya mshtakiwa na hatua ya kutolewa sababu ya dhamana hiyo kufungwa itaisaidia mahakama kupata mwongozo mzuri kabla ya kutoa uamuzi. Kuhusu kesi ya msingi, Jaji Fatma alisema kwamba itaendelea kusikilizwa kama kawaida licha ya upande wa mashtaka kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kupinga uamuzi wa Jaji Abraham Mwampashi juu ya uamuzi wake wa kufuta maamuzi yote yaliyotolewa na Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar na kuungana na uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka wa kufunga dhamana.

“Pamoja na upande wa mashtaka kukata rufaa bado hakuzuii Mahakama Kuu kusikiliza kesi ya msingi na tutaendelea kama kawaida baada ya kupokea sababu za DPP kufunga dhamana ya washtakiwa,” alisema Jaji Fatma.
Alisema kwamba suala la kukata rufaa ni haki ya msingi ya kila mtu kikatiba na kwamba hakuna sababu za msingi za kesi hiyo kusimama kusubiri maamuzi ya mahakama ya juu.

Kutokana na hali hiyo, Jaji aliutaka upande wa mashtaka uwasilishe kwa maandishi hoja za DPP kabla ya kesi hiyo kutajwa tena April 10, mwaka huu.
Awali Mwendesha Mashtaka kutoka ofisi ya DPP, Raya Mselem Issa, alidai kwamba taratibu za kukata rufaa tayari zimekamilika na kuomba mahakama kutojadili ombi la dhamana na kuitolea uamuzi hadi Mahakama ya Rufaa itakapotoa uamuzi wake.

“Ombi letu kesi isimamishwe hadi Mahakama ya Rufaa itakapotoa mwongozo, rufaa tuliyoikata kwa ajili ya kupinga maamuzi ya Jaji Mwampashi ya Machi 11, mwaka huu,” alidai Mselem. Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka tayari umekwisha kutaarifu mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Kesi hiyo inawahusu viongozi 10 wa Uamsho akiwamo Sheikh Farid Hadi Ahmed, Mselem Ali Mselem, Mussa Juma Issa, Azzan Khalid Hamdan, Suleiman Juma Suleiman, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakari Suleiman, Gharib Ahmada Omari, Abdallah Said Ali na Fikirini Majaliwa Fikirini.

Washtakiwa hao wamefunguliwa mashtaka ya uharibifu wa mali za serikali na kuhatarisha usalama wa taifa kinyume cha kifungu cha 3 (d) cha sheria ya Usalama wa Taifa sura ya 47 ya mwaka 2002 na kutoa lugha za uchochezi kinyume cha kifungu cha 11 cha sheria ya Usalama wa Taifa sura ya 47 ya mwaka 2002.
CHANZO::belteirass.blogsport.nl

INALILAH WAINA ILAYHI RAJIUN.


Hakika Sote ni wa Mwneyeenzi Mungu na marejeo yake ni kwake Napenda kuwatangazia kifo cha Sheikh wetu Rashid Nassor Al Batashi kilichotokea leo huko Hospitali ya Mnazi Mmoja na mwili wake utasaliwa katika Msikiti wa Jumuiya ya Waarabu Rahaleo baada ya sala ya Ijumaa na maziko yake yatafanyika nyumbani kwake Mlandege. Inshallah Mwenyeenzi Mungu amrahisishie safari yake na ampe kauli thabit. Ameeen

Monday 25 March 2013

DOGO KARIBU ATAITWA BABA 



HAPA VP DOGO ATAWEZA KUMUHUDUMIA MAMA ? 




                         Nyumba inauza ipo mtaa wa Mbweni njee kidogo wa mji wa zanzibar ,kwa mawasiliano zaid wasiliana nasi  www.beltelraas.blogspot.nl

ndo tumo ktk majiribio wapenzi wa blog lenu,mnajuwa tena test ,vitu huwa vinaingiya bila kuruhusiwa samahanini kwa yatakayo tokeya,

    Assallam alleykum
tunapenda kuwaarififu wapenzi ya blog au nyuzi kupitiya mitandaoni ,tumo ktk hatuwa zakuirekebisha blog yetu ili tuwe vizur na karibu na nyinyi,