Friday 28 June 2013

HATA BADO LAANATULLAHI BALOZI SEIF IDD !!!


MAKAMU wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd amehadharisha kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa inaweza kumeguka, iwapo viongozi wataendelea kutumia vibaya majukwaa ya kisiasa kwa kutoa kauli za chuki na matusi na kukashifu Serikali kwa maslahi binafsi.

Ingawa Balozi Idd alisema uhusiano wa viongozi wakuu watatu wa nchi ni mzuri: Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad na yeye Balozi Seif Ali Idd, wanafanya kazi vizuri.

Makamu wa Pili wa Rais, alikishutuma Chama cha CUF kwa kutumia majukwaa ya kisiasa vibaya. Alidai kinatumia lugha za matusi dhidi yake na kumpa majina mabaya.

Alisema kasoro kubwa zinajitokeza katika majukwaa ya kisiasa ambako viongozi wamekuwa wakitoa kauli za chuki zenye kutia wasiwasi mkubwa wananchi na kuhoji uhusiano wa viongozi hao kiasi cha kutukanana hadharani.

Akifanya majumuisho na kujibu hoja za Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliyochangia Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kwa mwaka ujao wa fedha juzi, Balozi Idd, alilaumu hususan viongozi wa CUF.

Maalim Seif ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, alisema katika mikutano yao yote wanayofanya, wamekuwa wakitumia vibaya majukwaa kumtukana yeye binafsi na kumchonganisha na wananchi na Serikali iliyopo madarakani.

“Napenda kuwaambia wananchi uhusiano wa viongozi wakuu wa Serikali ni mzuri sana…lakini majukwaa ya kisiasa yanatumiwa vibaya kutukanana…Tukiendelea hivyo hatufiki pahala na tutarudi tulikotoka,” alisema Balozi Idd.

Kwa mujibu wa Makamu wa Pili wa Rais, alisema amekuwa akipewa majina mabaya na viongozi wa CUF katika mikutano ya kisiasa; likiwemo ‘LAANATULLAHI’ wakimaanisha kumlaani. Jambo ambalo alisema anawauliza “amewakosea nini”?.

Balozi Idd, aliwahadharisha viongozi hao kwamba lengo la Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni kuleta mshikamano kwa Wazanzibari wote.

Alionya, kwamba watu wanaweza kurudi ambako walikuwa hawazikani wala kushirikiana katika matukio kutokana na siasa za chuki na uhasama kutawala tangu ulipoingia mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992.

“Tuache kutukanana katika hadhara za majukwaa ya kisiasa…Hawa CUF sijui nimewakosea nini na kama majina yanachuna basi tayari ngozi yangu ingeathirika,” alisema Balozi Idd.

Alikumbusha viongozi na wananchi kwamba kilichounganishwa ni Serikali yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa, lakini vyama vya siasa na sera ni tofauti na hakuna sababu ya kulumbana katika hilo.

Awali, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud alisema Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) iko kwenye mchakato wa kuboresha daftari la wapiga kura nchini kote.

Alitaka wanasiasa kujenga tabia ya kuwaamini watendaji wa taasisi hiyo na kuacha kuwahukumu kwa kuwashutumu, kitendo ambacho kinaweza kuzorotesha utendaji wa kazi hiyo.

“Tume hii imefanya kazi vizuri sana tangu mchakato wa kura ya maoni mwaka 2010 pamoja na kusimamia uchaguzi mkuu ambao ulikwenda vizuri na vyama vyote kuridhika,” alisema Aboud.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, iliundwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, 2010 kutokana na matakwa ya wananchi kupitia kura ya maoni na kushinda kwa zaidi ya asilimia 64.

Muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, unajumuisha Vyama vya CCM na CUF, ulifikiwa ili kuondoa siasa za chuki na uhasama katika visiwa vya Zanzibar.

Tuesday 25 June 2013

JUSSA ASEMA MAMLAKA KAMILI TU HAKUNA JENGINE !!!

Very interesting leo Mhe. Omar Yussuf Mzee alipokuwa akifanya majumuisho ya mjadala wa bajeti ya SMZ (wind-up of the budget speech) aliamua kuzinyamazia kimya na hakujibu kabisa hoja nilizozitoa jana kuhusu wizi wa mchana kweupe wanaotufanyia Tanganyika katika mafungu ya fedha za misaada ya kibajeti (GBS), fedha za mifuko ya miradi kisekta na fedha za miradi ya maendeleo zinazotoka kwa washirika wa maendeleo zinazoombwa na kutolewa kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ambazo ukifanya hesabu ya Zanzibar kupewa ule mgao wa 4.5% tu basi zinafikia TShs. 163 bn. 

Ukiacha hizo kuna na zile za mikopo ya elimu ya juu ambazo kama Zanzibar ikipewa 4.5% tu kutoka SMT basi ni TShs. 14.6 bn. wakati mahitaji ya Zanzibar kuwapatia mikopo wanafunzi wote wanaoomba ni TShs. 5 bn. 

Mbali ya hizo nilihoji gawio la Zanzibar kutoka taasisi za Muungano kama TCRA, TCAA, TTCL, TPC na TPDC ambazo zinakusanya mapato na nyingine Zanzibar ina hisa kabisa lakini hakuna tunachokipata. Chukulia mfano mdogo tu karibuni Vodacom peke yake ililipa TCRA kodi ya TShs. 36 bn. Je, ukichanganya na Zantel, Tigo na Airtel mbali na tozo na ada nyinginezo.

Ukiacha hizo hata kodi ya mapato (PAYE) inayotokana na wafanyakazi wa Taasisi za Muungano waliopo Zanzibar na ambao wanatumia huduma zote za hapa zinazolipiwa na walipa kodi wa Zanzibar nazo hazilipwi sawa sawa.

Halafu anatokezea mtu anasema Zanzibar inanufaika na mfumo uliopo wa Muungano na kwamba eti tunabebwa. Nani anambeba nani hapa? Nini faida ya Muungano wa aina hii?

Ndiyo maana tunasema hatupokei chochote pungufu ya MAMLAKA KAMILI ya Zanzibar kitaifa na kimataifa. Na tutahakikisha katika rasimu ya Katiba tunayarejesha kwenye mamlaka ya Zanzibar mambo yafuatayo ili tuweze kusarifu na kupanga uchumi wetu kwa maslahi ya nchi yetu na watu wetu. Mambo hayo ni:

1. Mambo ya Nje;
2. Sarafu na Benki Kuu; na
3. Uraia na Uhamiaji.

MWAKILISHI WA CCM ZANZIBAR NI RAIA WA KENYA ,JIMBO RAHALEO

Usitukane wakunga na uzazi ungalipo, iweje leo raia wa kenya anakuwa Mwakilishi wa CCM katika jimbo la rahaleo, ama kweli Muungano umetupandikizia wageni wengi kiasi watoke majasho Barazani kuutetea Muungano. 

Mmemuona Mhe Nassor Salim Ali Jazeera wa Kisauni Mombasa

UAMSHO ZANZIBAR !!!

TAARIFA YA JUMIKI KUHUSU TUKIO LA MUHADHARA WA MAHONDA TAREHE 21/06/2013 ALASIRI, JIONI

Siku ya Ijumaa tarehe 21/06/2013, askari walifika asubuhi mapema katika eneo la mahonda na kuwataka wenyeji wa wa eneo hilo kufunga maduka yao kwa kile walichokitaja kuwa hakutakuwa na muhadhara. Ilipofika majira ya saa 9:30 askari hao walifika na kuingia sehemu ya msikiti na kuwataka waislamu waliokuwa katika uwa wa msikiti huo kuingia ndani na kuanza kupachua bendera, tambara (lililokua na aya ya Mungu “walaa tahinuu walaa tahzanuu wa antumul a’launa inkuntum muuminiin) zilizokuwa zimepachikwa eneo hilo, maafisa 2 na askari 10 difenda waliendelea na vitisho vyao huku rova 4 zilizojaa askari wa FFU zikiuzunguka msikiti baada ya kuuziba mlango mkuu wa kuingilia ndani.

Mmoja miongoni mwa viongozi wa jeshi la polisi waliokuwa katika eneo hilo aliamrisha watu wapigwe mabomu na wamwagiwe maji, amri ambayo haikutekelezwa kwa wakati huo na askari waliokuwapo eneo la tukio.

Sambamba na hilo, Jeshi la polisi Zanzibar, mkoa wa kaskazini walisema uongo kwa kumdanganya Imamu wa msikiti wa mahonda kwa kumwambia kuwa wamekubaliana na kamati ya msikiti muhadhara usiwepo kitu ambacho kamati imekikanusha.

JUMIKI inatamka yafuatayo kutokana na tukio hilo:

1. Tunaalaani vikali kitendo cha jeshi la polisi - Zanzibar kuingia eneo la msikiti na kuwatisha waumini waliokusanyika kwa amani kwa lengo la kusikiliza muhadhara huo ilhali wakiwa hawajafanya fujo wala kubeba silaha ya aina yoyote.

2. JUMIKI inalaani kitendo cha jeshi la polisi - Zanzibar kuvamia eneo la msikiti na kushusha bendera tukufu ya Uislamu yenye shahada ya LAA ILAAHA ILLA ALLAH MUHAMMAD RASUULULLAH, nine ambalo ni nguzo ya kwanza ya Uislamu. Kitendo hicho si tu kinadhalilisha Jumuiya ya kiislamu ya Uamsho, bali pia kinaudhalilisha Uislamu na Waislamu kwa ujumla.

3. JUMIKI inalaani kitendo cha jeshi la polisi – Zanzibar kwa kumdanganya kiongozi wadini na kwa kufanya kazi kwa kufuata utashi wa kisiasa badala ya sheria na kanuni za kazi zao.

4. JUMIKI itaendelea na mihadhara ya kuuelimisha Umma wa kiislamu na haitatishwa na vitimbi vya watu wasiomjua Mungu wala wasioheshimu kanuni wala sheria hata zile walizozitunga wenyewe na kuzilia viapo wasivyovitekeleza.

Wabillah Taufiq

Imetolewa na:
OFISI YA KATIBU MKUU
JUMIKI, ZANZIBAR
14 Shaaban, 1434.
24/Juni/2013

Thursday 13 June 2013

DADA NA KAKA SEX DAR ES SALAAM


UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni. Usemi huu unakamilishwa na tukio la kunaswa kwa vijana wawili wenye undugu wa damu wakifanya mapenzi   kando ya Ufukwe wa Bahari ya Hindi

Imefahamika kwamba vijana  hao, kaka na dada   wamenaswa ‘wakingonoka  katika mapango yaliyopo kando ya Ufukwe wa Coco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.


Tukio zima lilitokea mchana kweupe wa saa 9 na kudhihirisha habari za mara kwa mara zinazoeleza kwamba Ufukwe wa Coco umekuwa ukitumika kwa ufuska usiku na mchana.

Beltelraas  lilinasa tukio hilo kwa kutumia mitambo maaalum iliyoelekezwa kando ya bahari.

Wawili hao walinaswa tangu walipokuwa wakiingia katika ufukwe huo na kuwafuatilia nyendo zao, hatua kwa hatua.

 Haikufahamika mara moja kama wawili hao walikuwa na makubaliano ya kwenda kuduu katika ufukwe huo au la, lakini kwa mbali ilionekana kama vile dada mtu alikuwa akizingua kwenda kutenda dhambi hiyo.

Picha za video zilizonaswa, zinamuonesha dada huyo akionekana kutoa upinzani pale alipokuwa akishikwashikwa na kaka yake.

Alionekana kama vile hakuwa tayari kwa mchezo huo.
Hata hivyo, kaka mtu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23-26 alikuwa akilazimisha kitu fulani ambacho kilionekana dhahiri kupitia kamera zetu.
Ni kama vile hawakuwa na makubaliano na kile walichokuwa wakienda kukifanya.

Mara kadhaa dada huyo alionekana kumkwepa kaka yake na alikuwa akijiondoa karibu yake pale alipomlazimisha kutaka kumfanyia kitu kisichokuwa cha kawaida.

Kamera za Beltelraas ziliwafuatilia wawili hao kwa kuwa walionekana kuwa na kitu ‘spesho’.

 Mpaka wanazama katika mapango yaliyopo kando ya ufukwe huo wa Coco, kamera zilikuwa zikiendelea kuwachukua hadi walipozama ndani kabisa ya mapango hayo. 

Walipozama ndani ya mapango hayo, ghafla walitokea askari ambao nao walikuwa wakifuatilia nyendo za wawili hao.

Askari hao wa Kituo cha Oysterbay, wakiongozwa na kamanda wa oparesheni maalumu katika Wilaya ya Kinondoni, Kamanda Swai walifuatilia kwa umakini tukio hilo.

Wakiwa chini ya mapango, kaka na dada waliondoa vinguo vilivyokuwa maungoni mwao na kuanza kuduu kama vile walikuwa katika ufukwe unaoruhusiwa kufanya vitendo hivyo.

Kabla askari hawajawavamia, waliwashuhudia wawili hao wakiwa katika kilele cha sterehe yao huku dada mtu akionesha kutoa ushirikiano kwa shingo upande.

Ghafla, askari waliwavamia na kuwatibulia starehe yao kisha kuwatia mbaroni.

Baada ya kuona kuwa wamevamiwa na askari, kaka mtu alichomoka na kutafuta silaha ili kuweza kujihami na wavamizi wake bila ya kujua kama ni askari.

Katika hilo nusura zipigwe kati ya askari na kaka huyo ambaye alikuwa akitaka kupigana na watu asiowajua kwa kuwa walikuwa wametinga mavazi ya kiraia.

Hata hivyo, alitulizwa na kutakiwa kuvaa pensi yake ili aweze kutoa maelezo kwa kina. 

Wakati yote yakiendelea, dada mtu alikuwa amepigwa na butwaa na kutojua cha kufanya hadi aliporushiwa kitenge chake kilichokuwa pembeni ili ajisitiri mwili wake.

Katika mahojiano ya awali yaliyoongozwa na Kamanda Swai, ilibainika kwamba wawili hao ni ndugu wa damu yaani kaka na dada. 

Maelezo hayo yanasema kuwa dada mtu alitoka mkoani na alikuja kutembea jijini Dar es Salaam, ndipo kaka yake alipomtaka watoke kwenda kumuonesha vivutio vya jiji hilo.

“Nina miaka 19, nimetokea Iringa kuja Dar kutembelea familia lakini kaka akanileta huku na kunifanyia vile, siyo kama tulikuwa tumekubaliana,” alisema dada huyo kwa aibu.

Kaka mtu alikiri kile kilichosemwa na dada yake na kushindwa kujitetea kwa kuwa kila kitu kilikuwa hadharani.


Wawili hao walichukuliwa na kupelekwa katika Kituo cha Oysterbay kwa ajili ya kufunguliwa kesi ya uzembe na uzururaji na kusekwa rumande kabla ya kufikishwa mahakamani.

MUUNDO WA MUUNGANO HUU HAURIZISHI !!!

JAJI mstaafu Joseph Warioba na Tume yake ya Mabadiliko ya Katiba wametamka na wananchi wamewasikia. Jumatatu walimkabidhi Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal rasimu ya kwanza ya katiba mpya ya Tanzania waliyoipendekeza na Bilal akaizindua.
Wazanzibari walikuwa wakiisubiri kwa hamu na ghamu rasimu hiyo wakitaka kujua nini Tume itapendekeza kuhusu muundo wa Muungano. Kwa muda mrefu tumekuwa tukisema kwamba mchakato wa kulitafutia taifa la Tanzania katiba mpya lazima utaibadili sura ya Muungano na hautokuwa kama ulivyokuwa tangu uasisiwe.
Kwa mfano, tukisema kwamba haielekei ya kuwa Tume ya Warioba itapendekeza kuendelezwa kwa mfamo wa sasa uliopo wa serikali mbili za Muungano na Zanzibar. 
Wala Tume isingelithubutu kupendekeza kuwako kwa mfumo wa serikali moja tu, mfumo ambao lazima ungeleta mpasuko mkubwa nchini humo. Pangalitolewa pendekezo hilo basi nina hakika kwamba pasingelikalika.
Tumekuwa tukisema kwamba wengi wa Wazanzibari wamechoshwa na mfumo uliopo wa Muungano na wakitaka ubadilishwe na pawe na Muungano wa mkataba badala ya huu uliopo wa Katiba. 
Kuna wengine ambao wanasema wamechoshwa kabisa na Muungano wenyewe na wanataka Zanzibar iachiwe ijitoe.  Hisia kama hizo pia wanazo baadhi ya watu wa Bara ingawa si zenye hamasa nyingi kama za Wazanzibari.
Wazanzibari, si wote lakini wengi wao, wamekuwa wakiupigia debe muundo wa Muungano utaoirejeshea Zanzibar mamlaka yake kamili ya kidola. Wamekuwa pia wakidai ifufuliwe rasmi ile iliyokuwa Tanganyika na ipewe nayo serikali yake na mamlaka yake kamili ya kidola.
Wazanzibari hao wamekuwa wakishikilia kwamba Muungano mpya uwe ni Muungano wa mataifa mawili yaliyo sawa kila moja likiwa linashughulikia mambo yake yenyewe kwa ukamilifu.
Kwa mfumo huo wa Muungano Zanzibar bado itapunjika.  Muungano ulikuwa na nguvu zaidi ya hizo kwa muda wa takriban miaka 50 na Zanzibar haikupata natija ya maendeleo kama inavyostahiki.
Sijui kwa nini rasimu hii ya katiba inaziita nchi hizi mbili Tanzania/Bara na Tanzania/Zanzibar badala ya Tanganyika na Zanzibar. Kwa nini ionekane jambo la aibu kulifufua jina Tanganyikana kulipa hadhi yake na taifa hilo kupewa haki yake ya kuwa na serikali yake na utaifa wake?
Kabla ya kuja dhana ya Muungano wa Mkataba wengi wa Wazanzibari walikuwa wakipendekeza kuwa Muungano uwe na muundo wa serikali tatu. Pendekezo hili liliwahi kutolewa na Rais wa pili wa Zanzibar Sheikh Aboud Jumbe na wakati mmoja hiyo ndiyo iliyokuwa sera ya Chama cha Wananchi (CUF).
Rasimu hii ya kwanza iliyozinduliwa Jumatatu imependekeza kuwa Muungano wa Tanzania uwe na muundo wa serikali tatu.  Pawepo na Serikali ya Tanzania/Bara, serikali ya Tanzania/Zanzibar na serikali ya shirikisho.
Aidha yale yaitwayo ‘mambo ya Muungano’ yamepunguzwa kutoka 22 na sasa kuwa saba.  Hayo saba ni:
  • Katiba ya Jamhuri ya Muungano
  • Sarafu na Benki Kuu
  • Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa
  • Ushuru
  • Ulinzi na Usalama
  • Usajili wa vyama vya siasa na
  • Uraia na uhamiaji.
Mambo haya saba ya Muungano yaliyopendekezwa kwa hakika ni mambo ambayo kwa jumla unaweza kuyaita kuwa ndiyo mambo yenye ‘nguvu za mamlaka.’ Kwa mantiki hiyo iwapo mambo hayo na nguvu hizo saba zitabakia katika Muungano, Zanzibar bado haitokuwa na mamlaka yake kamili. 
Kinachofanyika hapo ni sawa na kile kilichofanywa na serikali ya kikoloni ya Uingereza ilipoipa Zanzibar serikali ya ‘madaraka ya ndani.’ Na tunaweza kuhoji kwamba serikali hiyo ya madaraka ya ndani ilikuwa na nguvu zaidi na hiyo inayopendekezwa na Tume ya Katiba kwa vile ilikuwa na wizara ya mambo ya ndani ya nchi.
Nimejaribu kutafuta maoni ya Wazanzibari kuhusu rasimu hii ya kwanza ya katiba na ninavyoona ni kwamba wengi wao wanasema kwamba mabadiliko hayo yaliyopendekezwa hayatoshi. Wanasema kwamba hayatoshi kwa sababu hayakidhi madai ya Wazanzibari wengi.
Hawasemi kwamba mabadiliko hayo hayana maanalakini wanachosema ni kwamba mabadiliko hayo bado yataufanya Muungano uidhibiti Zanzibari ilhali wanachotaka wao ni kupumua.
Mbali na ya Muungano kuna mengi yenye maana katika rasimu hii yanayopaswa kuungwa mkono.  Kwa mfano, Tume ya Katiba imependekezwa kwamba Katiba itoe haki ya kuyahoji matokeo ya uchaguzi wa urais katika mahakama ya juu zaidi. 
Tume imependekeza pia kwamba mshindi wa urais atangazwe iwapo atapata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa.
Jengine la kihistoria lililopendekezwa na Tume ni kwamba wagombea binafsi waruhusiwe kuwania viti vya toka ngazi za chini hadi cha urais.  Pendekezo hili likikubalika litaitanua demokrasia nchini.
Jengine lenye maana lililopendekezwa na Tume ni kwamba idadi ya mawaziri wa Muungano isizidi 15 na mawaziri hao kabla ya kuzishika nyadhifa zao lazima kwanza waidhinishwe na Bunge la Muungano.
Kwa upande mwingine, mapendekezo yaliomo kwenye rasimu hii ya katiba yanaonyesha wazi kwamba sera ya CCM imeshindwa ya kutaka uendelezwe muundo wa Muungano wa serikali mbili. 
Hivyo ni wazi pia kwamba msimamo wa Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na ule wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, umepitwa na wakati.  Warioba na Tume yake wameling’amua hilo.
Kuna tofauti kubwa kati ya Tume hii ya Warioba na zile za Nyalali na Kisanga. Katika mchakato huu wa sasa kuna mabaraza ya katiba ambayo hayakuwepo wakati wa tume zilizotangulia. Jambo jingine muhimu ambalo limo katika mchakato wa sasa na ambalo halikuwepo kabla ni rasimu ya mwisho ya katiba itapigiwa kura na wananchi ili waamue iwapo wanaikubali au la.
Kwa hivyo, uamuzi wa mwisho hautokuwa tena katika mikono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano kama ilivyokuwa wakati wa enzi za Mwalimu Julius Nyerere na Benjamin Mkapa. 
Wala CCM hakitokuwa na uamuzi. Sasa uamuzi utakuwa wa wananchi. Wao ndio watakaoamua hatima ya Muungano na muundo wake.
Hatua itayofuata sasa katika mchakato wa kupata katiba mpya ya Tanzania ni kwamba rasimu hii ya kwanza ya katiba itabidi ijadiliwe na wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya. 
Mijadala hiyo itafanyika baadaye mwezi huu bado mwezi wa Agosti mwaka huu. 
Baada ya kupata maoni ya mabaraza hayo, Tume itakaa tena kuyatafakari maoni hayo na kuyaingiza katika rasimu ya mwisho ya katiba ambayo itawasilishwa mbele ya Bunge la Katiba.  Baada ya hapo ndipo wananchi watapotakiwa waipigie kura rasimu hiyo katika kura za maoni zitazopigwa mwakani 2014.
Ikiwa rasimu hii ya sasa ya katiba ndiyo itayoibuka na kuwa ya mwisho ya kupigiwa kura na wananchi na kukubaliwa basi nina hakika kwamba huo utakuwa mfumo wa mpito tu. 
Bado pataendelea kuwako na manung’uniko Zanzibar kwa vile wengi wa wananchi wa huko hawatoridhishwa na muundo huo wa serikali tatu uliopendekezwa katika rasimu hiyo. Lengo lao ni kutaka pawe na Muungano wa Mkataba.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/muundo-wa-muungano-bado-hauridhishi#sthash.S7HKU84R.dpuf

Sunday 9 June 2013

WAZANZIBAR WAANZA KUIGA CCM BAADA YA KUKOSA MWELEKEO YA KUDAI ZANZIBAR YENYEWE MAMLAKA KAMILI !!!





Mamiya ya wasuasi wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar huko matemwe wamemkabizi Maalim Seif Sharif Hamad zao za CCM na kujiunga na Wazanzibar wenziwao kudai Zanzibar yenye mamlaka kamili ,
 Kiasi cha watu mia saba wamekabidhiwa kadi za CUF na makamo wa kwanza wa raisi wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad baada ya kubaini kwamba chama cha CCM kimeshindwa kutetea maslahi ya Zanzibar katika mchakato wa mabadiliko ya katiba na badala yake kimekuwa kikiutetea ukoloni wa Tanganyika dhidi Zanziabar

Wednesday 5 June 2013

MPAKA KIWELEWEKEE!!!

TANGAZO LA DUA MAALUM

Jumuiya ya UAMSHO na Mihadhara ya Kiislamu-Zanzibar inapenda kuwatangazia Waislamu wote wanawake na wanaume kua, kutasomwa DUA MAALUM siku ya Ijumaa tarehe 07 Juni, 2013 katika msikiti wa Darajabovu-Bati jekundu, mara baada ya sala ya Ijumaa insha Allah.

Lengo la DUA hii ni kumuomba Mwenyezi Mungu awape Shekhe zetu ithbati kwa dhulma wanazofanyiwa na kuwa na subira pamoja na familia zao katika wakati huu mgumu. Dua hii itasomwa vile vile katika mikoa yote ya Unguja na Pemba Inshaa Allah. Shime sote tuhudhurie.

TUNATAKA ZANZIBAR YETU HURU, YENYE MAMLAKA YAKE KAMILI, KITAIFA NA KIMATAIFA
WABILLAH TAUFIQ

UAMSHO MEDIA CENTER
24 Rajab, 1434 – 05 Juni, 2013
Email: jumiki@hotmail.com
Facebook: Uamsho Zanzibar
Twitter: @Uamsho1

Monday 3 June 2013

KUHUSU RASIMU MPYA YA KATIBA (BAADHI YA MAMBO YALIYOMO) ISOME YOTE HAPA - NYUMBA YA HABARI

KUHUSU RASIMU MPYA YA KATIBA (BAADHI YA MAMBO YALIYOMO) ISOME YOTE HAPA - NYUMBA YA HABARI

SAFARI YA KUELEKEA MAMLAKA KAMILI IMEPIGA HATUA KUBWA: !!!



Mamlaka ambayo tayari Zanzibar itakuwa imeyarejesha kwa kuondolewa kwenye Muungano kupitia Rasimu ilotangazwa leo ni:

1. Polisi.

2. Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje.

3. Kodi ya Mapato.

4. Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.

5. Mabenki ya Kibiashara na Fedha za Kigeni.

6. Leseni ya viwanda na takwimu.

7. Elimu ya Juu.

8. Maliasili ya mafuta na gesi asilia.

9. Baraza la Taifa la Mitihani.

10. Usafiri na usafirishaji wa anga.

11. Utafiti.

12. Utabiri wa Hali ya Hewa.

13. Takwimu.

14. Mahkama ya Rufani.

15. Ushirikiano wa Kimataifa.


KAZI ILIYOBAKI KWA WAZANZIBARI ILI KUTIMIZA MAMLAKA KAMILI

Ni kutumia hatua zilizobakia kuyarejesha pia mamlaka katika mambo muhimu yafuatayo:

1. Mambo ya Nje.

2. Uraia na Uhamiaji.

3. Sarafu na Benki Kuu.

4. Ushuru wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa.

5. Usajili wa Vyama vya Siasa.


TANBIHI:
Wananchi na hasa Vijana wa Zanzibar tumefikia hatua ya kurejesha mamlaka katika mambo hayo 15 kutokana na umoja wetu na kutumia njia za amani huku tukiwa na msimamo usiyoyumba. Tuendelee kuwa pamoja, tukitumia njia za amani kabisa kukamilisha mamlaka kamili tunayoyataka.

Naiona ileeeee.........
SAFARI YA KUELEKEA MAMLAKA KAMILI IMEPIGA HATUA KUBWA: 

Mamlaka ambayo tayari Zanzibar itakuwa imeyarejesha kwa kuondolewa kwenye Muungano kupitia Rasimu ilotangazwa leo ni:

1. Polisi.

2. Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje.

3. Kodi ya Mapato.

4. Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.

5. Mabenki ya Kibiashara na Fedha za Kigeni.

6. Leseni ya viwanda na takwimu.

7. Elimu ya Juu.

8. Maliasili ya mafuta na gesi asilia.

9. Baraza la Taifa la Mitihani.

10. Usafiri na usafirishaji wa anga.

11. Utafiti.

12. Utabiri wa Hali ya Hewa.

13. Takwimu.

14. Mahkama ya Rufani.

15. Ushirikiano wa Kimataifa.


KAZI ILIYOBAKI KWA WAZANZIBARI ILI KUTIMIZA MAMLAKA KAMILI

Ni kutumia hatua zilizobakia kuyarejesha pia mamlaka katika mambo muhimu yafuatayo:

1. Mambo ya Nje.

2. Uraia na Uhamiaji.

3. Sarafu na Benki Kuu.

4. Ushuru wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa.

5. Usajili wa Vyama vya Siasa.


TANBIHI: 
Wananchi na hasa Vijana wa Zanzibar tumefikia hatua ya kurejesha mamlaka katika mambo hayo 15 kutokana na umoja wetu na kutumia njia za amani huku tukiwa na msimamo usiyoyumba. Tuendelee kuwa pamoja, tukitumia njia za amani kabisa kukamilisha mamlaka kamili tunayoyataka.

Naiona ileeeee.........

Saturday 1 June 2013

ZANZIBAR LAZIMA IWE NA URAIA WAKE!!!

Zanzibar. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad amesema muundo wowote utakaokuja wa Muungano lazima Zanzibar iwe na mamlaka kamili ya kidola.
Alisema kinyume na mamlaka kamili rasimu itakayokuja itakataliwa bila ya kigugumizi.
Maalimu Seif Sharif Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUf) aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Kibandamaiti Zanzibar.
“Wazanzibar wapatao asilimia 66 wametoa maoni yao yenye mamlaka kamili, leo uje na katiba inayokwenda kinyume na matakwa yao, hilo halikubaliki” alisema Maalim Seif.
Akizungumza juu ya mambo ambayo hayapaswi kuwa ya Muungano alisema ni pamoja na uraia, uhamiaji, sarafu, mipaka, polisi na mambo ya nje.
“Tanganyika watoe Pasi za kusafiria zao na Zanzibar zao” alisema Hamad.
Mapema mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu alisema hatarajii kama Tume ya Mabadiliko ya Katiba itapanga maoni ya vongozi wengi wa Juu Tanzania ya kuipa Zanzibar Mamlaka yake.