Saturday 1 June 2013

ZANZIBAR LAZIMA IWE NA URAIA WAKE!!!

Zanzibar. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad amesema muundo wowote utakaokuja wa Muungano lazima Zanzibar iwe na mamlaka kamili ya kidola.
Alisema kinyume na mamlaka kamili rasimu itakayokuja itakataliwa bila ya kigugumizi.
Maalimu Seif Sharif Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUf) aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Kibandamaiti Zanzibar.
“Wazanzibar wapatao asilimia 66 wametoa maoni yao yenye mamlaka kamili, leo uje na katiba inayokwenda kinyume na matakwa yao, hilo halikubaliki” alisema Maalim Seif.
Akizungumza juu ya mambo ambayo hayapaswi kuwa ya Muungano alisema ni pamoja na uraia, uhamiaji, sarafu, mipaka, polisi na mambo ya nje.
“Tanganyika watoe Pasi za kusafiria zao na Zanzibar zao” alisema Hamad.
Mapema mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu alisema hatarajii kama Tume ya Mabadiliko ya Katiba itapanga maoni ya vongozi wengi wa Juu Tanzania ya kuipa Zanzibar Mamlaka yake.

No comments:

Post a Comment