Monday 8 April 2013

MAFUTA WAZANZIBAR KUYATOWA KWENYE MUUNGANO !!!




SERIKALI ya Zanzibar imesema kamati maalum ya wanasheria wakuu wa serikali imeundwa kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi wa mwisho suala la mafuta na gesi, kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano.
Hayo yalisemwa na waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Pili wa rais Zanzibar, Mohamed Aboud alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Muyuni, Unguja aliyetaka kujua, lini kero za Muungano zitapatiwa ufumbuzi, likiwemo suala la mafuta na gesi.
Waziri Aboud alisema suala la mafuta na gesi ambalo SMZ, kupitia azimio la Baraza la Wawakilishi, wanataka liondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano, lipo katika hatua ya ngazi ya vikao vya wanasheria wakuu wa serikali zote mbili:
“Suala hili sasa wameachiwa wanasheria wakuu wa pande mbili za serikali ya Muungano na Zanzibar, kwa ajili ya kulifanyia kazi katika ngazi ya kisheria, na wananchi wanatakiwa kuwa watulivu,” alisema Aboud.
Alisema suala ma mafuta na gesi, tangu awali ni mambo ambayo yamo katika orodha ya Muungano kwa mujibu wa Katiba ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akiwa London, mwezi wa August mwaka 2011 alisema suala la mafuta na gesi ya Zanzibar, ni miongoni mwa mambo yaliyopelekwa kwenye Muungano tangu mwaka 1966 kwa ridhaa ya serikali zote mbili.
Alisema ni kweli serikali ya Zanzibar, imeamua mafuta na gesi ya Zanzibar, yaondoshwe kwenye serikali ya Muungano, lakini alisema chombo ambacho kinapaswa kuridhia suala hilo ni Bunge la Muungano.
Dk Shein alisema yeye mwenyewe (SHEIN) anazo kumbukumbu za Bunge ‘HANSARD’ za vikao vya Bunge vya mwaka 1966, zinazoeleza kuwa suala la mafuta ni la Muungano na ili kulitoa kunahitaji utaratibu wa kisheria, ufuatwe.
Aidha, kupitia mkutano wake na viongozi wa Jumuiya ya Wazanzibari, wanaoishi nchini Uingereza (ZAWA) Dk Shein, aliwatoa shaka Wazanzibari, juu ya suala hilo, kwa sababu alisema ni jambo linalozungumzika na ana imani ufumbuzi, utapatikana.
Akifafanua ndani ya Baraza la Wawakilishi jana, Waziri Aboud alisema tangu kuundwa kwa kamati ya kuzipatia ufumbuzi kero za Muungano mwaka 2006, jumla ya kero 13 zimejadiliwa na kero sita tayari zimepatiwa ufumbuzi.
Alizitaja baadhi ya kero ambazo zimepatiwa ufumbuzi: “Tume ya haki za binadamu na utawala bora, kuwepo kwa mfuko wa Jimbo pamoja na kuruhusiwa kwa Zanzibar, kukopa kutoka taasisi za fedha nje ya Tanzania”.
Pia, alizitaja kero zinazoendelea kufanyiwa kazi: “Mgawanyo wa mapato yanayotokana na Benki kuu, ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kuachana na kuwa kwenye kivuli cha mwenvuli wa Muungano wa Tanzania, kama ilivyo sasa”.
Akifafanua kwa undani: Alisema katika suala la mfuko wa pamoja wa fedha, Serikali ya Zanzibar tayari imetoa mapendekezo yake katika mgawanyo wa fedha na kwa sasa inasubiri serikali ya Muungano, kupitia kikao cha Baraza la mawaziri:
“Zanzibar inataka iingie ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa hadhi ya nchi kamili na sio kutumia mwenvuli wa Muungano wa Tanzania,” aliongeza Waziri Aboud.
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inaundwa na nchi tano kwa sasa, ikiwa ni pamoja na Tanzania Bara (Tanganyika) iliyojibebesha na Zanzibar. Nyengine ni Burundi Rwanda, Kenya na Uganda.
Akiwahutubia wananchi mwaka 1970, kwenye bustani za Manispaa (sasa Karume House) Rais wa kwanza wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, Marehemu mzee Abeid Aman Karume, aliwambia Wazanzibari wakiona koti la Muungano linawabana, watalivua..

No comments:

Post a Comment