Monday 8 April 2013

JK AKUMBUKA KUMTEMBELEYA ABOUD JUMBE MWINYI

Rais Jakaya Kikwete, jana alimtembea na kumsalimia aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mzee Alhaj Aboud Jumbe nyumbani kwake Mji Mwema, jijini Dar es Salaam.

Rais Kikwete, ambaye alifuatana na mkewe, Salma, alitoka moja kwa moja Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam baada ya kutua akitokea Zanzibar na kupanda kivuko eneo la Feri na kwenda kumwona Mzee Jumbe.

Rais Kikwete alikuwa Zanzibar kushiriki dua ya kumbukumbu ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume.

Rais Kikwete alizungumza na Mzee Jumbe kwa muda ambapo Mzee huyo alimwambia Rais kuwa hali yake ni nzuri na afya yake ni imara.

Mzee Jumbe alikuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu Aprili,1972 kufuatia kuuawa kwa Mzee Karume na akawa Makamu wa Rais wa Tanzania tangu mwaka 1977 chini ya Baba wa Taifa, hayati Julius Kamba Nrage Nyerere,

Viongozi wengi wa  chama na serekali walimtenga Mzee Jumbe kutokana na msimamo wake wa kuwa na serekali tatu katika Jahmuri ya Muungano ,

No comments:

Post a Comment