Tuesday 23 April 2013

KIKWETE AINGIZWA CHEO CHA KIKE HALIMA MDEE CHADEMA !!!



Suala la mbegu zenye Viwatilishi (GMOs), limeibuliwa tena bungeni na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee aliyeitaka Serikali kujiuliza zaidi kabla ya kuruhusu kampuni za kigeni kuleta mbegu hizo.
Mdee alisema kutokana na athari zake kwa ardhi na binadamu, watoto ambao wazazi wao wamekula mazao yake wanazaliwa wakiwa taahira.
Akichangia bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mdee alisema baadhi ya kampuni za mbegu hizo tayari zimefukuzwa nchini India na Amerika kutokana na madhara ambayo wananchi wake waliyapata kwa sababu ya kutumia teknolojia hiyo.
“Mosanto (Kampuni za mbegu zenye Viwatilishi), imefukuzwa India kwa sababu iliwafanya wakulima wadogo kuwa maskini zaidi, iliwafanya wakulima kutegemea mbegu kutoka kwake kila mwaka, kwa sababu hizi mbegu zikishapandwa mara moja hauwezi kurudia tena,” alisema Mdee.
Alisema kampuni hiyo imekubali kusaidia Afrika kwa mamilioni ya fedha, huku majaribio ya mbegu za pamba nchini tayari yakiwa yameanza.
Mbunge huyo alisema Ufaransa imeifukuza kampuni hiyo kwa madai kuwa, watoto wanaokula chakula kinachozalishwa na mbegu hizo wanazaliwa wakiwa taahira.
“Yawezekana Rais akaingizwa choo cha kike na hawa mabeberu, kama huko Ulaya wenzao wamewakataa kwa nini sisi tuwakubali, wengi wenu hapa mna zaidi ya miaka 50 msituharibie kikazi hiki, baraza la mawaziri mshaurini vizuri Rais,” alisema Mdee.
Alisema kampuni hiyo ambayo inaonyesha nia ya kuja kuwekeza nchini,imefukuzwa Argentina na Peru kutokana na kubainika kuwa mbegu hizo hazimsaidii mkulima wala udongo.

Pia,alitaka kuangalia upya suala la kutoa ardhi kwa wawekezaji nchini, kwani linaweza kufanya wananchi wengine kukosa ardhi ya kutosha.
Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya (CCM) aliitaka Serikali kuhakikisha inatumia kilimo kama njia ya kupunguza tatizo kwa vijana.
Bulaya alisema kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee kuna asilimia 30 ya vijana wasio na ajira, 15 kwenye miji mingine na asilimia saba vijijini.
“Huku vijijini inaonekana hivi kwa sababu vijana ndiyo hao wamekimbilia Dar es Salaam... Serikali iangalie suala hili kwa umakini,” alisema.
Pia, alitaka kutumia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuzalisha chakula na kwamba, suala hilo litafanya nchi kuwa na chakula mpaka cha kuuza nje tofauti na sasa.
“Hizi kambi 15 za JKT zikitumika vizuri tutakuwa hatuna tatizo la chakula, kule kuna vijana wengi wanakwenda kwa mujibu wa sheria na wengine kwa kujitolewa, wakimaliza wanarudi mitaani, hawa watumike kuzalisha chakula,” alisema.

No comments:

Post a Comment