Friday 26 April 2013

KWA NIONAVYO MIMI !!! SEREKALI YA TANGANYIKA NA UDINI !!!

Kwa nionavyo mimi: ila kubwa ambalo waislamu wamekua wakilalamikia ni upendeleo wa serikali kwa wakristu huku ikiwaacha waislamu. angalieni mifano ifuatayo;
1- waislamu wamekua wakilalamikia serikali kutotambua siku ya ijumaa kama siku ya ibada. wakristo wana jumapili lkn waislamu waliyo wengi wamekua wakishindwa kufanya ibada kutokana na ijumaa kuwa siku ya kazi. wameomba pia kama inawezekana angalau saa 5 na nusu hadi saa nane uwe muda rasmi wa kuwaruhusu waislamu kwenda kufanya ibada siku za ijumaa. la ajabu hadi bunge huendelea na mijadala mida ya adhuhuri siku za ijumaa.
2- waislamu wamekua wakilalamikia upendeleo uliyofanywa na serikali kwa kuingia mkataba na TEC na CCT. mkataba huo unajulikana kama MEMORANDUM OF UNDERSTANDING. waislamu wanajiona kama mtoto ambaye anawekwa kando huku kaka yake akiendelezwa kwa kupewa mtaji wa biashara.
3- waislamu wamekua wakilalamikia kutopata fursa ya kuwa na mahakama za kadhi zinazotambulika rasmi kikatiba. wamefafanua kuwa mahakama a kadhi itahusu mirathi, ndoa, talaka na wakfu. mambo ya jinai hayamo kwenye mahakama ya kadhi. licha ya mambo haya kuwa IBADA kwa waislamu, wakristo wamekataa katakata uanzishwaji wa mahakama ya kadhi. waislamu kwa upande wao wameona kuwa wanaingiliwa katika ibada yao. wametoa mifano kuwa uganda. afrika ya kusini, uingereza nk... kuna mahakama za kadhi licha ya hizi nchi kuwa na idadi ndogo za waislamu.
4- waislamu waliwahi kushauri nchi yetu ijiunge na oic. walieleza faida za kujiunga na oic kiuchumi. wakristo wakamekataa suala la oic. wanasema nchi haina dini. haiwezi kusajiliwa kuwa ya kiislamu. uganda, msumbiji nk... ni wanachama wa oic.
5- waislamu wamelalamikia NECTA kuwa na viongozi wakristo watupu. hakuna muislamu pale. muislamu kama yupo atakua mfagiaji. mwaka juzi na jana, ilibainika kuwa watoto wa kiislamu walifelishwa mtihani wa islamic knowledge. NECTA walikira na kusema kuwa ni kosa la kikompyuta. hakuna akiejiuzulu!
6- waislamu wamelalamikia kuwekwa kando katika ajira ya umma. wanasema kuwa wakristo ni wengi maofisini. wanaendelea kubebana licha ya kuwepo waislamu wenye sifa. baadhi ya ofisi za serikali zinaonekana kama parokia. wameombwa pawe na mpango mkakati wa kuwachomeka kwenye ajira serikalini (wenye sifa) ili angalau nao washiriki katika matunda ya keki ya taifa.
7- waislamu wanasema wamekua kwa miaka mingi wakichukuliwa kama minority group. ktika sensa ya mwaka jana, waliomba kiwekwe kipengela cha sensa ili ukweli wa idadi ya watu kidini ujulikane. walitoa mfano kuwa inasemekana wakristo ni wengi. hivyo, inapopangwa mipango ya maendeleo kwa mfano ardhi kwa ajili ya nyumba za ibada na maziko, wakristo hupewa maeneo makubwa kwa madai kuwa ni wengi.
8- waislamu wamekuwa wakilalamika kuwa nchi yetu inaendeshwa kwa mfumo kristo. wanasema kipindi cha sikukuu, ofisi za serikali hupambwa muda wa sikukuu za wakristo. sikukuu za waislamu hakuna kinachofanyika!
9- kama ulivyo sema, waislamu wanalalamika kuwa serikali imekua ikiikumbatia sana BAKWATA na kudharau taasisi nyingine za kiislamu. BARAZA KUU ni taasisi yenye waislamu wengi hapa nchini kuliko bakwata. serikali huwa haiipi taasisi ya baraza kuu uzito wowote.
UFAHAMU WANGU :
kundi katika jamii linaposononeka kwa muda mrefu, hukata tamaa. baada ya kukata tamaa kupoteza imani na serikali yao. waislamu wanaamini kuna urafiki mkubwa kati ya serikali na ukristo. hali hii inawafanya wawachukie wakristo wakiwaona kuwa wabaya wao. hoja ya kusema rais, makamu, rais na wakamu wawili wa znz, igp, jaji mkuu kuwa wote ni waislamu haina mashiko. hawa siyo watendaji mkoa, wilaya, kata hadi kijiji. mfumo wanasema ni wakikiristo. hata kama viongozi wa juu watakua waislamu, hilo ni kiini mamcho.

nashauri upande wa wakristo watambue na kutafakari madai ya waislamu kuliko kuwadhihaki kuwa "wala ubwabwa hao, wavaa kanzu hao, wavaa msuli hao..........". kuwadhihaki ni kungeza mpasuka ambao unafanya amani na umoja vizidi kutoweka.

No comments:

Post a Comment