Thursday 25 April 2013

MAANDAMANO LONDON MBELE YA UBALOZI WA SAUDIA !!!



Maandamano London mbele ya ubalozi wa Saudia
Makumi ya watu mbalimbali wakiwemo Waislamu waishio nchini Uingereza, wamefanya maandamano mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia wakipinga hakumu ya kutaka kunyongwa mwanazuoni wa Saudia sheikh Nimr Baqir al-Nimr. Maandamano hayo yamefanyika leo mjini London, Uingereza. Katika maandamano hayo yaliyowashirikisha Waislamu wa Bahrain, Saudi Arabia, India, Pakistan na Iraq, waandamanaji walitoa nara za kulaani utawala wa Aal Saudi, kuwa ni muenezaji wa ugaidi duniani. Aidha waandamanaji wamesisitiza juu ya kukomeshwa uingiliaji wa masuala ya ndani ya Bahrain sambamba na kutaka kuachiliwa huru mwanazuoni huyo anayeendelea kuzuiliwa katika korokoro za Aal Saudi. Aidha waandamanaji hao waliokuwa wamebeba mabango mbalimbali, wamelaani vikali uungaji mkono wa Rais Barack Obama wa Marekani kwa utawala wa Saudia. Katika maandamano hayo Said al-Shahabi, Mkuu wa Kituo cha Tamaduni mjini London amesema kuwa, maisha ya Sheikh Nimr Baqir al-Nimr yako hatarini na kwamba, Marekani na Uingereza kwa kuziunga mkono tawala za Bahrain za Saudia zinahusika moja kwa moja katika umwagaji damu wa raia wasio na hatia  na wapigania uhuru duniani.

No comments:

Post a Comment