Wednesday 8 May 2013

MAKAAZI YA POLISI ZANZIBAR NOMA NYUMBA ZAO ZINANUKA!!!


Dodoma. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imekiri kuwa makazi ya Polisi katika Mkoa wa Pemba si ya kuridhisha na yanakabiliwa na changamoto nyingi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Pereila Ame Silima ambaye alisema tatizo la ubovu wa nyumba za Polisi lipo kwa nchi nzima na kwamba uhaba wa fedha katika bajeti ndiyo sababu.
Naibu Waziri huyo alitaja baadhi ya maeneo ya vituo na makazi ya Polisi hao ambayo ndiyo yenye changamoto zaidi ya mazingira kuwa ni pamoja na Ziwani, Mwera, Bububu na Chakechake ambavyo viko mkoani Pemba.
Alikuwa akijibu swali la Mwanakhamis Kassim Said (Viti Maalumu-CCM),aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kufanyia ukarabati nyumba za askari ambazo zimechakaa sana maeneo hayo.
Naibu Waziri alisema ni azma ya Serikali kuboresha makazi ya watumishi wote wakiwamo polisi lakini akasema kazi hiyo inafanywa kwa awamu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Hata hivyo alishindwa kujibu moja kwa moja ni lini hasa ukarabati wa nyumba hizo utafanyika.

No comments:

Post a Comment