Monday 13 May 2013

DUNI-TUSIPOKUWA MAKINI MUUNGANO UTATUMALIZA WAZANZIBAR !!!


Wananchi mbali mbali wa Zanzibar wametakiwa kushikamana kwa umoja wao hadi pale nchi yao itakapokuwa na huru wake wakujitegemea.

Kauli hio imetolewa na mkurugenzi wa haki za binadamu,habari,uenezi na mawasiliano ya umma wa chama cha wananchi CUF Mh,Salim Biman katika mkutano wa hadhara uliofanyika huko Jimbo la Magomeni uwanja wa Mzalendo.

Katika mkutano huo ambao jumla ya wananchama wapya 63wapya wamekabidhiwa kadi za chama hicho na mgeni rasmi katika mkutano huo Mh,Juma Duni Haji.

Biman amesema kuwa katika suala la harakati za kudai Zanzibar huru kwamba wazanzibar hawataki malumbano juu ya hili lakini wakiamua kulumbana itakuwa hapatoshi “sisi ni wazalendo wa nchi yetu tunapodai Zanzibar huru hakuna makosa kama wanaumwa wataumwa sana mwaka huu’’alisema Bimani.

Pia alitolea mfano kaulia ya Raisi wa kwanza wa Taifa hili la Zanzibar, Mzee Abeid Amani Karume ambayo mara kwa mara alikua akitumia wakati wa uhai wake kwa kusema “huwezi kuwa mwana wa nchi ikiwa huna uchungu na nchi yako,niwajibu wako uitete na kupigania nchi yako huo ndio utu na huo ndio uzalendo’’alifahamisha Biman.

Nae Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni Mh,Nassor Ahmed Mazrui ambae pia ni waziri wa biashara viwanda na masoko amesema,hivi karibuni nchi zetu hizi mbili ziliadhimisha sherehe za muungano ambapo uhalisia kabisa sherehe hizo hazikuwa za muungano kwa upande wa Zanzibar bali nisherehe za dhiki zinazotokana na mungano huu unaiokandamiza nchi hii kwa kila hali.

Ameleza kwamba yeye binafsi na wazanzibar wengine kuwa wanaimani tume ya mabadiliko ya katiba mpya wamejua kwa kina hasa nini wazanzibar wanataka juu ya nchi yao licha ya kuwepo baadhi ya watu kwa makusudi waliokuwa na lengo la kutaka kuvuruga mchakato huo kwa maslahi yao binafsi.

Amesema katika hatuwa hii ya pili ya mchakato wa katiba mpya kila mzanzibari anapaswa kujua kuwa hakuhitajiki jazba bali kunahitaji hoja madhubuti ambazo zitawafanya wahusika wa tume hio kujua nini wazanzibar wanataka.

Pia amefahamisha kuwa yoyote yule atakaetoa maoni kwa tume hio kwa ajili ya chama chake na sio kuiweka nchi yake mwanzo basi mtu huyo haitakii mema Zanzibar bali anataka kuipeleka nchi pabaya na kuizamisha zaidi.

Pia Bwana Mazrui amefahamisha kwa kusema kuwa mfumo huu wa muungano uliopo hauna kero wala changamoto badala yake una kasoro na iwapo kasoro hizi ziliopo hazitoondolewa basi muungano huu hauna maisha tena.

“Ni lazima katiba mpya inayokuja idhinishe mamlaka sawa ya kila nchi kwani mfumo huu wa muungano ulikosewa kabisa kwa kule kutoa haki kwa upande mmoja tu watanganyika”alisema Mazrui.

Akizungumzia kuhusu suala la mambo mbali mbali ya muungano ambayo wazanzibari wananyimwa fursa wakati na wao niwashiriki wakuu wa muungano.

Alitolea mfano wizara yake ya biashara viwanda na masoko kuwa sio jambo la muungano lakini cha kushangaza hawezi kufanya lolote lile ikiwa ni kusaini mkataba wowote wa maendeleo kwa Zanzibar kupitia wizara yake kama haujasainiwa Bara.

Licha ya sheria ya Zanzibar kusema kuwa Wazanzibar wenyewe wanahaki ya kuamua nini wanataka nini hawataki lakini chakushangaza wamekuwa wakiamuliwa.

“Katiba mpya ni lazima iweke bayana yepi ni mambo ya muungano na yepi si ya muungano ili kuondosha mtafaruki kwa wazanzibar,pia ni lazima iondoe kasoro zote ziliopo ndani ya muungano”alifafanua Mazrui.

Nae mgeni rasmi katika mkutano huo Mh,Juma Duni Haji amesema kuwa chama cha CUF kinapofanya mikutano yake lengo kuu kabisa ni kuwaelimisha wasiofahamu nini wazanzibar wanataka juu ya nchi yao.

Amesema kuwa niwajibu wao kama viongozi ndio wanaotakiwa kuwataarishia vijana wanaokuja mazingira mazuri ya maisha yao na sio kama hivi wanavoishi hivi sasa kutokana na nchi ya Zanzibar kubanwa kila njia za uchumi na Tanganyika.

“Mimi binafsi nimekwisha sina umri mrefu tena lakini je vijana wanaokuja tutawajengea mustkbali gaini wa maisha yao ikiwa hali itaendelea kuwa hivi’’alieleza Duni.

Katika hali ya kushangaza ambayo ipo kwa baadhi ya watu wengi sana katika jamii yetu wanadhani kuwa katiba mpya imekuja tu kirahisi,ila ukweli haikuja tu hii wenzetu wana lengo lao ambalo wameliweka tayari na nikuimaliza Zanzibar kabisa na hatimae kuwa mkoa.

Na hali hii imekuja baada ya Nyerere kutokuweza kulitimiza lengo hili wakati wa uhai wake na ndio maana sasa kina Warioba na Butiku wanataka kutumia kila njia kulitimiza lengo hili ,lakini tusipokuwa makini wazanzibar juu ya njama zao hizi wanaweza kufanikiwa.

Ameleza kuwa wakati wa uhai wake Nyerere mara kwa mara alijaribu kuhakikisha kuwa hakuna kabisa Taifa linaloitwa Zanzibar na ndio maana akachukua madaraka ya Karume kwa kuhofia pale Karume atakaposimama nje ya nchi na kusema yeye ni Raisi wa Jamuhuri ya Zanzibar basi ingeishusha hadhi Tanganyika.

Pia amefahamisha kwamba watanganyika wenyewe wanajua wazi kuwa utajiri wa nchi unatokana na wananchi wenyewe kumiliki biashara zao lakini wapi wamejimilikisha kila kitu unadhani kweli nchi hii itapata maendeleo chini ya muungano huu uliopo.

Pamoja na hayo ameleza kutokana na Zanzibar kuwa katika kipindi kigumu sana cha njaa wakati huo ndio Nyerere akatumia muda huo kwa kuja na njama maalumu ya kuunganisha nchi huku akijua kuwa wazanzibar kwa hali waliokuwa nayo hawatokataa kabisa kuunganisha nchi yao na Tanganyika.

Mnamo mwaka 1965 chama cha TANU tayari kilikuwa ni chama cha serikali lakini wakanyamaza kimya na mnamo mwaka 1977 ndio Nyerere kwa ujanja wake akaja na njama zake za kuunganisha vyama na hatimae akafanikiwa kutokana na chama cha TANU kikatawala nchi nzima.


“Lakini pia Nyerere hakuridhika licha ya hatua yake ya kuchanganya nchi kufanikiwa kwani alijua wazi kuwa nguvu ya wazazibar ni chama chao cha ASP hivo alitumia kila njama kuhakikisha anakiuwa chama hicho ili kuwagawa wazanzibar makundi tofauti ‘’chakushangaza nyinyi hadi leo hii mnabaki kidumu kidumu yagujuu’’alifafanua Duni.

Mnamo mwaka 1964 wazee wetu walipindua nchi hii kwa lengo la kujitawala wazanzibar wenyewe na sio kutawaliwa na kufanywa kuwa kuloni na lawatanganyika kama ilivo hivi sasa.

“Sasa la kujiuliza ndugu zangu ikiwa nyerere katufikisha hapa hivi munadhani ninani kwa upande wa Tanganyika atakuwa na imani na sisi huku Zanzibar,muda umefika wazanzibar tujikomboeni na muungano huu unatumaliza”alisema Juma Duni.

Aidha amefahamisha kwamba ndugu zetu wa Tanganyika ni wabaya mno ni mara ngapi wametugombanisha wazanzibari sisi kwa sisi tena bila wenyewe kujijua.

Sambamba na hayo ameleza kuwa wananchi wa Zanzbar wanapaswa kuelewa kuwa kwa sasa wakati umefika wakuikomboa nchi yao kwa hali na mali kwani kazi iliobakia si ya CUF wala CCM bali ni yawazanzibar wote kuidai nchi yao mpaka wahakikishe ipo huru na yenye kujitgemea.

No comments:

Post a Comment