Wednesday 8 May 2013

HUKMU YA SHEIKHE PONDA NI LEO !!!


HATIMA ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 inatarajiwa kujulikana leo wakati Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itakapotoa hukumu katika kesi ya uchochezi na wizi wa mali inayowakabili.
Kesi nyingine inayotarajiwa kutolewa hukumu yake leo ni ile ya kupinga uamuzi wa kuvuliwa ubunge kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga. Dk. Peter Kafumu (CCM).
Kesi ya Ponda
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Victoria ndiye atakayetoa hukumu hiyo baada ya kushindwa kufanya hivyo Aprili 18, mwaka huu na hatimaye ikaahirishwa hadi leo.
Tanzania Daima imedokezwa kuwa Jeshi la Polisi limeimarisha zaidi ulinzi ndani na nje ya viwanja vya mahakama hiyo ili kudhibiti vurugu zozote zinazoweza kutokea.
Aprili 3, mwaka huu, mawakili wa upande wa Jamhuri, Tumaini Kweka na Jessy Peter na mawakili wa utetezi, Juma Nassor na Njama waliwasilisha majumuisho yao mahakamani hapo kwa njia ya maandishi huku mawakili wa Jamhuri waliiomba mahakama iwatie hatiani na kuwapa adhabu washitakiwa.
Mawakili wa utetezi waliiomba mahakama isiwatie hatiani washitakiwa na iwaachie huru kwa sababu hawakutenda makosa yanayowakabili na kwamba upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi yao.
Oktoba 18, mwaka jana, Ponda na wenzake walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza ambapo Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka alidai washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa matano.
Makosa hayo ni kula njama kinyume cha kifungu 384 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2012, kwamba Oktoba 12 mwaka jana, huko eneo la Chang’ombe Markazi washitakiwa wote walikula njama kwa nia ya kutenda kosa hilo.
Shitaka la pili, wakili Kweka alidai linawakabili washitakiwa wote ambalo ni la kuingia kwa nguvu kwa nia ya kutenda kosa kinyume cha kiufungu cha 85 na 35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu na kwamba Oktoba 12, mwaka jana, huko Chang’ombe Markazi, kwa jinai wasipokuwa na sababu za msingi washitakiwa waliingia kwenye kiwanja kinachomilikiwa na Kampuni ya Agritanza Ltd kwa nia ya kujimilikisha kiwanja hicho isivyo halali.
Shitaka la tatu ni kujimilikisha kiwanja, shitaka la nne ni la wizi, ambalo ni kinyume cha kifungu cha 258 cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, na kuwa kati ya Oktoba 12-16 mwaka jana, washitakiwa hao waliiba vifaa na malighafi, matofali 1,500, nondo na tani 36 za kokoto, vitu vyote hivyo vikiwa na thamani ya sh milioni 59.6 mali ya Kampuni ya Agritanza Ltd.
Shitaka la tano ni la uchochezi ambalo linamkabili Sheikh Ponda peke yake, ambalo ni kinyume cha kifungu cha 390 na 35 cha sheria hiyo, kwamba kati ya Oktoba 12-16 mwaka huu katika eneo hilo la Chang’ombe Markazi kwa maelezo kuwa yeye ni Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) aliwashawishi wafuasi wake ambao ni washitakiwa hao kutenda makosa hayo.
Igunga
Hukumu ya kupinga uamuzi wa kuvuliwa ubunge kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga, Peter Kafumu (CCM) inatarajiwa kutolewa leo na jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa mjini Tabora.
Rufaa hiyo iliyokatwa na Mwanasheria wa Serikali kupinga maamuzi yaliyomvua ubunge Kafumu itatolewa uamuzi na majaji watatu ambao ni Nathalia Kimaro, William Mandia na Semistrocles Kaijage.
Wakili wa serikali, Gabriel Malata, katika hoja zake anataka uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumvua ubunge Dk. Kafumu utenguliwe kwa madai Jaji aliyesikiliza kesi hiyo alikosea kuisikiliza, kwakuwa mlalamikaji hakutimiza matakwa ya kisheria.
Malata alidai kuwa mlalamikiwa hakulipa ada ya mahakama kiasi cha shilingi milioni moja alizotakiwa kutoa au hati ya nyumba kabla kesi hiyo haijaanza kusikilizwa kama sheria ya uchaguzi kifungu namba 111 inavyoelekeza.
Wakili Malata aliongeza kuwa kwa vile mjibu Rufaa, Joseph Kashindye na wenzake hawakutekeleza sharti hilo usikilizwaji wa shauri hilo pamoja na mwenendo mzima yakiwamo maamuzi vyote vilikuwa ni batili.
Aliongeza kuwa hata ushahidi uliotolewa wakati kesi hiyo iliposikilizwa na Jaji Shangali ulikuwa ni wa kusikia, hivyo siyo wa kutiliwa maanani, hivyo aliwaomba majaji hao watengue uamuzi ya Mahakama Kuu.
Hoja hizo na nyingine zilipingwa na wakili wa mjibu rufaa Profesa Abdalah Safari ambaye aliitaka Mahakama ya Rufaa kuzitupilia mbali kwa sababu mahakama iliyosikiliza kesi hiyo iliridhika na ukiukwaji wa sheria uliofanyika wakati wa zoezi zima la uchaguzi wa Jimbo la Igunga.
Rufaa hiyo inafuatia maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotengua matokeo ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga mkoani hapa baada ya kubainika kuwa uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya rushwa, kampeni chafu na vitisho dhidi ya wapiga kura.
Jaji Mary Nsimbo Shangali wa Mahakama Kuu alitangaza kutengua matokeo hayo baada ya mahakama hiyo kuridhika na hoja saba kati ya 17 zilizowasilishwa na upande wa mlalamikaji, Joseph Kashindye na wenzake na uamuzi ukatolewa Agosti 21, mwaka jana.
Kesi hiyo ilifunguliwa na mlalamikaji aliyekuwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye aliwakilishwa na wakili maarufu nchini, Profesa Abdallah Safari, ambapo alipinga matokeo ya uchaguzi huo akilalamikia kukiukwa kwa sheria ya 

No comments:

Post a Comment