Mahakama Kuu ya Zanzibar imetupilia mbali ombi la mtuhumiwa wa mauaji ya Padre Evarist Mushi, la kupinga kukamatwa na kushikiliwa kwa zaidi ya saa 24 bila ya kupelekwa mahakamani, kutokana na ombi hilo kufunguliwa kinyume na sheria za Zanzibar.
Mtuhumiwa Omar Mussa Makame (35), alifungua ombi hilo mahakamani kupitia jopo la mawakili wanaomtetea Abdallah Rajab Abdallah na Abdallah Juma Mohamed.
Mawakili hao walikuwa wakipinga kitendo cha Jeshi la Polisi Zanzibar kumkamata mtuhumiwa huyo Machi 17, mwaka huu na kufikishwa mahakamani Aprili 5, mwaka huu.
Akisoma hukumu baada ya kusikiliza ombi hilo, Jaji wa Mahakama Kuu, Mkusa Isaack Sepetu, alisema ombi hilo lilifunguliwa kinyume na kifungu cha nne Sura ya 28 cha Sheria ya Zanzibar.
Aidha, Jaji Mkusa alisema maombi hayo yameonekana kuwa na tarehe mbili tofauti, ikiwamo mwezi Machi na Aprili na hivyo kuipa wakati mgumu mahakama kufahamu ni tarehe ipi ambayo hati ya kiapo ilifunguliwa kabla ya kusikilizwa na kutolewa uamuzi wake.
“Kutokana na kasoro hizo za kisheria, maombi hayo hayakuwa na nguvu za kisheria, kujadiliwa na kutolewa maamuzi na kwa msingi huo, Mahakama imeyatupa,” alisema Jaji Mkusa.
Hata hivyo, wakati hukumu hiyo inasomwa, mawakili wote wanaomtetea mshtakiwa huyo hawakuwapo na wakati Jaji Mkusa, akijitayarisha kupanga tarehe ya kutajwa kesi ya msingi, wakili kutoka kampuni ya A.J.M Shaban Juma Shaban, alifika ghafla katika ukumbi wa mahakama na kuitaka mahakama kurejea hatua ya mwenendo wa kesi ilipofikia.
Jaji Mkusa aliwataka mawakili hao kuwa makini wanapotekeleza majukumu yao, kwa vile kampuni hiyo ina mawakili wengi na hakukuwa na sababu za msingi za kutofika wakili hata mmoja wakati wakifahamu kesi ya msingi itatajwa pamoja na kutolewa hukumu ya ombi la mteja wao.
“Natoa nafasi kwa upande wa Mwendesha Mashitaka, kurudia maelezo aliyoyatoa mahakamani kuhusu kesi ya msingi, lakini tabia hiyo iwe mwanzo na mwisho,” alisema Jaji Mkusa.
Aidha, Jaji Mkusa aliwataka mawakili hao kutorudia hoja wanazoziwasilisha mahakamani na kutolewa uamuzi ili kuepusha mahakama hiyo kuwa kama gurudumu la kujadili mambo ambayo yameshajadiliwa na kutolewa uamuzi wake.
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili Shabani kutaka mahakama hiyo imwachie huru mtuhumiwa huyo kama upelelezi bado haujakamilika pamoja na kutaka Mmhakama iwape muda maalum wa kuhakikisha upelelezi unakamilika, hoja ambazo zimewahi kuwasilishwa na Wakili Abdallah Juma Mohamed Aprili 19, mwaka huu.
Awali, Mwendesha Mashitaka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Abdallah Issa Mgongo, aliieleza mahakama hiyo kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Mgongo alisema uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika na hivyo kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine ya kusikilizwa kwa shauri hilo, lakini wakati akitoa maelezo hayo mawakili wa mtuhumiwa hawakupo katika ukumbi wa mahakama hiyo.
Jaji Mkusa aliiahirisha kesi hiyo hadi Mei 9 mwaka huu na kuwataka wahusika wote kuhakikisha wanafika kwa wakati ili kuepusha usumbufu wowote kama ulivyojitokeza jana.

![KWA NINI UISLAMU UMEHARAMISHA WANAUME KUVAA DHAHABU NA HARIRI?
Leo ulimwenguni kote kutokana na kile kinachojulikana kama wimbi la kwenda na wakati, uhuru na haki ya mtu kufanya/kuishi atakavyo; si jambo la kushangaza wala kustaajabisha kuwaona vijana wa kiume wakiwa wamejipamba kwa kuvaa mikufu, pete na hata hereni za dhahabu. Hili leo si geni tena bali ni jambo la kawaida na fakhari hata katika miji ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, ambako asilimia kubwa ya wakazi wake ni wafuasi wa dini ya Kiislamu kwa miongo ya miaka. Uvaaji huu wa dhahabu kwa vijana wa kiume umeingizwa pande zetu hizi za Afrika ya Mashariki na vijana waliotoka huku kwenda nchi za Ulaya kutafuta ajira hasa ya ubaharia. Hawa waliporejea wakiwa wameuiga utamaduni huo wa kigeni na kuwaathiri vijana wengine, limbukeni wenye kuiga kila kiingiacho mjini.
Utamaduni huu wa vijana wa kiume kujipamba kwa kuvaa dhahabu unakwenda kinyume na utamaduni wa mila ya Kiislamu. Mwenyezi Mungu amemuumba mwanamume na Mwanamke na kumpa kila mmoja maumbile na tabia zinazotofautiana na mwenzake. Ikiwa hili linaashiria kitu, basi si kingine bali ni kutofautiana pia katika nafasi na majukumu ya kila mmoja wao. Nadharia inaonyesha kuwa tabia na maumbile ya mwanaume ni ukakamavu na ugumu, wakati ambapo tabia na maumbile ya kike ni ulaini na ulegevu. Uislamu unamtaka mwanaume alelekee katika mazingira yaliyo mbali na udhaifu,unyonge na anasa zinazoweza kunlegeza ili aweze kuwa imara na mwenye nguvu katika kupambana na harakati za maisha ya kila siku, ambapo sehemu kubwa ya jukumu hilo amebebeshwa yeye na sheria . Sasa kwa kuzingatia kuwa madini ya dhahabu na hariri ni vitu vya anasa ambavyo humfanya mvaaji aonekane amependeza machoni mwake yeye mwenyewe kwanza na machoni mwa wengine na natija yake ni kuvaana na maumbile ya kupendeza ambayo ni ulaini na ulegevu. Pengine kwa njia moja au nyingine hii ndio inaweza kuwa hekima/falsafa ya kuharamishwa dhahabu na hariri kwa wanaume kwa kuwa inakubaliana na tabia na maumbile yao.
Hebu tujaribu kuwa wakweli, tuwatie katika mizani ya haki na uadilifu wanaume wenye kuvaa dhahabu na wasiovaa dhahabu, tutagundua nini? Bila ya shaka mtakubaliana na mimi kuwa ipo tofauti ya dhahiri baina yao, wavaao dhahabu watakuwa wameathirika na tabia na maumbile ya kike. Taathira hii utaiona katika mwendo wao, uzungumzaji wao, uvaaji wao na wakati mwingine huiga hasa tabia za kike kama vile kusuka nywele na kutumia vipodozi.
Ni kweli usiopingika kwamba kujua hekima/falsafa ya kuharamishwa dhahabu na hariri kwa wanaume, hii ni elimu isiyo na manufaa na ni ujinga usiodhuru. Usiulize hekima kwa kuwa kumeshurutishwa katika kuulizia hekima ya amri au makatazo, awe huyo muamrishaji/mkatazaji analingana sawa na kufanana na huyo muamrishaji/mkatazwaji na hapa ni suala la Mungu Muumba Muamrishaji na mwanadamu kiumbe muamrishwa. Kwa mantiki hii mwanadamu hana budi kuikubali na kuipokea amri kwa kuwa Mola wake ameamrisha/amekataza,kisha baada ya kutekeleza aliloamrishwa ndipo anaweza kutafuata kujua hekima/falsafa ya amri ile. Lakini kule kujua hekima/falsafa iliyomo katika amri au katazoisiwe ni sharti ambalo kwanza ni lazima litimizwe kabla ya kuamrika au kukatazika. Muislamu wa kweli anaambiwa na Mola wake:
“HAIWI KWA MWANAUME ALIYEAMINI WALA KWA MWANAMKE ALIYEAMINI, ALLAH NA MTUME WAKE WANAPOKATA SHAURI,WAWE NA HIARI KATIKA SHAURI LAO. NA MWENYE KAMUASI ALLAH NA MTUME WAKE, HAKIKA AMEPOTEA UPOTOFU ULIO WAZI (kabisa) [33:36]
Kuharamishwa uvaaji wa dhahabu kwa wanaume kumethibiti katika hadithi nyingi sahihi zilizopokelewa kutika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu –Rehema na Amani zimshukie.
1. Amepokea (riwaya) Imamu Bukhaariy, Muislam na Ahmad kwamba Mtume wa Allah “Amekataza (kuvaa) pete ya dhahabu”.
2. Imepokelewa kutoka kawa Ibn Abbaas-Allah awawiye radhi-kwamba Mtume wa Allah aliiona pete ya dhahabu kidoleni mwa mtu, akamvua na kuitupa (huku) akisema “ Mmoja wenu analikusudia kaa la moto na kulivaa mkononi?” Mtu yule akaambiwa baada ya kwenda zake mtume “ Itwae pete yako unufaike nayo. Akawajibu Wallah hapana, kamwe sitaichukua ikiwa aliyeitupa ni Mtume wa Allah –Rehema na Amani zimshukie.” Muislam
3. Na katika jumla ya riwaya zilizopokelewa kwamba Mtume wa Allah –Rehema na Amani zimshukie amesema : “ Ye yote mwenye kumuamini Allah na siku ya mwisho basi asivae hariri wala dhahabu.” Al-musnad {Musnadul–Imam Ahmad}
HITIMISHO
“AMA YULE ALIYEASI NA AKAYAPENDA ZAIDI (maisha) YA DUNIA. BASI KWA HAKIKA JAHANAAM NDIYO ITAKAYOKUWA MAKAZI YAKE. NA AMA YULE ALIYEOGOPA KUSIMAMISHWA MBELE YA MOLA WAKE, AKAIKATAZA NAFSI YAKE NA MATAMANIO (maovu). BASI HUYO PEPO NDIO ITAKAYOKUWA MAKAZI YAKE”. {79:37-41}.
Ndugu yangu mpenzi, chagua na uamue sasa, uvae dhahabu kwa kupata starehe na burudani ya muda mfupi ya duniani huku ukisubiriwa na adhabu kali ya milele ya akhera au uishinde nafsi yako na kuacha kuvaa dhahabu ewe mtoto wa kiume ukapate starehe ya kweli, ya kudumu ya akhera.](https://fbcdn-photos-b-a.akamaihd.net/hphotos-ak-frc1/384460_377572865676142_1265374836_s.jpg)